Ajiriwa.net English

Kuhusu sisi

Ajiriwa.net ni tovuti ambayo ilitengenezwa ili kurahisisha zoezi zima la uajiri kwa kuwaunganisha waajiri moja kwa moja na watafutaji wa kazi na kurahisisha mawasiliano kati yao.

Ajiriwa.net kama jina lake linavyojieleza imetengenezwa na kuongozwa na Peter Robert Mgembe ambae alikuwa na maono ya kubadilisha mfumo mzima wa uajiri.

Kabla ya kuanzishwa tovuti hii shughuli nyingi za uajiri zilifanywa na madalali ambao walifanya makubaliano na waajiri kutafuta wafanyakazi pale wanapohitajika. Njia hii haikuwa na ufanisi kwa kuwa haimpi mwajiri uhuru wa kuchagua kutokana na ukweli kwamba machaguo ni machache. Ajiriwa.net inaleta watu wanaotafuta kazi katika sehemu moja na hivyo kumwezesha mwajiri kuwa na uhuru wa kuajiri mtu anayekidhi mahitaji, lakini pia kwa watafutaji wa kazi inaziweka nafasi zote za kazi pamoja ili kurahisisha upitiaji na hivyo kufanya chaguo sahihi.

Jinsi mfumo unavyofanya kazi

Kwa kutumia mfumo huu waajiri wanaweza kupata maombi moja kwa moja kutoka kwa wanaotafuta kazi kulingana na kazi wanazochapisha. Maombi haya yanawekwa pamoja katika kurasa moja ambayo mwajiri anaweza kupitia kirahisi na kuweza kuona CV za wale wote waliofanya maombi. Hii ni njia rahisi ya kuweza kujua ni mtu yupi anafaa.

Mwajiri anaweza kuwasiliana na muhusika kwa urahisi kwa kutuma ujumbe ndani ya mfumo huo, hivyo wataweza kuokoa muda na fedha kwa kuwa hakutokuwa na hitaji la madalali.