Bodi ya chama cha ushirika wa akiba na mikopo Lulu(Lulu Saccos Ltd) MBR.737 kilichopo Jiji la Mbeaya maeneo ya Soweto kata ya Ruanda kinatoa tangazo la kazi kwa nafasi zifuatazo:-
Karani wa Fedha - Nafasi 1
Sifa
- Awe na umri kuanzia miaka 23 hadi 35
- Awe na Elimu ya sekondari
- Awe na stashahada ya uhasibu, ushirika na fedha ktuoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali
- Awe ni mtanzania anayeishi katika jiji la Mbeya
- Awe hajawahi kupatikana na kosa la jinai
- Awe ni mtu wa kujituma
- Awe ni mtu anayejisimamia mwenyewe
- Awe anajua kutumia kompyuta
- Awe ni mzaliwa wa mkoa wa Mbeya
Kazi
- Kutunza na kuangalia wakati wote kasiki la chama
- Kutunza vitaby vya fedha
- Kupokea fedha taslimu
- Kulipa malipo mbalimbali
- Kufanya malinganisho ya fedha ya kila siku kwa kushirikiana na mhasibu msaidizi
- Kuhakiki hati za benki kabla ya kukatia stakabadhi
- Atafanya kazi zingine zozote atakazopangiwa na mwajiri wake
- Kuandaa taarifa za fedha za kila siku
- Awe ni mzaliwa wa mkoa wa Mbeya
KAZI HII NI YA KUJITOLEA KWA MUDA WA MIEZI MITANO(5) BAADA YA HAPO ATAAJIRIWA KAMA ATAKUWA AMEKIDHI VIGEZO
Utaratibu wa kuomba
- Mwombaji anatakiwa kuambatanisha picha mbili passport size
- Mwombaji atatakiwa kuambatanisha vivuli vya vyeti vya kuzaliwa na vya masomo
- Mwombaji aambatanishe CV yake wakati wa kuomba kazi
- Mwombaji aonyeshe mawasiliano yake bayana
- Mwombaji atakayefaulu kwa awamu ya kwanza ataitwa kwenye usaili
- Mwombaji atakeyeitwa kwenye usaili aje na vyeti halisi siku ya usaili
- Mwombaji atajigharamia mwenyewe wakati wa usaili
- Maombi yatumwe kwa:-
MWENYEKITI WA BODI
CHAMA CHA USHIRIKA WA AKIBA NA MIKOPO LULU
S.L.P 3467
MBEYA