Shule ya St Jude inapenda kuwaalika kuhudhuria mnada wa hadhara wa vitu vipya na vilivyotumika
Tarehe: Jumamosi 1 Novemba 2025
Muda wa kufika na kutazama vitu: 2:30 asubuhi – 3:30 asubuhi
Muda wa mnada: 3:30 asubuhi– 5:30 asubuhi
Eneo la tukio: St Jude’s Sisia Campus, Moshono, Arusha
Kwa mawasiliano: Aimable Karamaga - 0716676537
Lister Gerald- 0755534741
Trekta
Matairi ya magari
Vifaa vya Gereji
Betri
Printa
Vitabu
Laptop
Kompyuta, Monita na Kipanya
Ngoma
Nyaya
Vipande vya mbao
Vyuma
Tenki
Viti
Kuingia na Kutazama Bidhaa: Washiriki wataruhusiwa kuingia geti la shule kwa ajili ya kutazama bidhaa na maandalizi kati ya saa 2:30 asubuhi na saa 3:30 asubuhi pekee. Baada ya muda huu, geti litafungwa ili kuanza mnada.
Kuanza kwa Mnada: Mnada utaanza saa 3:30 asubuhi ukiongozwa na MC.
MC ataanza na Lot ya kwanza na kuendelea hadi lot ya mwisho.
Kwa kila lot, MC atatangaza bei ya kuanzia iliyowekwa na kamati ya mnada.
Uendeshaji wa mnada:
Washiriki wataweka dau lao kwa uwazi hadi mshindi wa mwisho atakapopatikana.
Mwakilishi wa St Jude ataandika majina ya mshindi mwenye dau kubwa na wa pili kwa mujibu wa tangazo la MC kabla ya kuendelea na lot inayofuata.
Malipo na Utoaji wa Risiti: Washindi wa mnada wataenda moja kwa moja kwa timu ya fedha mara baada ya kutangazwa, kwa ajili ya kufanya malipo, kupokea risiti,makabithiano na kupata kibali cha getini cha kutoa bidha/vitu alivyoshidwa kwenye mnada.
Kuchukua Bidhaa: Washindi wote wanatakiwa kuchukua bidhaa walizonunua kati ya saa 6:30 mchana na saa 9:00 alasiri siku hiyo-hiyo, chini ya usimamizi wa wafanyakazi wa St Jude.
Malipo yote ni lazima yafanyike mara moja (100%) baada ya mshindi kutangazwa.
Iwapo mshindi atashindwa kulipa, mshiriki aliyekuwa wa pili kwa dau kubwa atatangazwa kuwa mshindi mpya.
Bidhaa zote zilizolipiwa lazima zichukuliwe siku hiyohiyo ya mnada.
Kushindwa kuchukua bidhaa kutasababisha bidhaa hizo kutaifishwa na Shule ya St Jude, na hakutakuwa na marejesho ya fedha (HATUREJESHI PESA).
Hakutakuwa na maegesho ndani ya kampasi. Tafadhali egesha gari nje ya lango bila kufunga njia kuu ya kuingia.
Shule ya St Jude inahifadhi haki ya kughairi sehemu yoyote au mnada mzima wakati wowote kabla au wakati wa mnada, na pia haina wajibu wa kueleza sababu za ughairishaji wowote.
Kwa Maelezo zaidi Fungua Hapa