Dereva
Kiswahili
Dereva

Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi

Website
ajira

Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi ni taasisi ya serikali ambayo imeanzishwa kwa sharia Na. 4 ya mwaka 2010. Mojawapo ya majukumu yake ni kusajili na kuratibu wabunifu majengo, Wakadiriaji Majenzi na Wataalamu wanoshabihiana nao.

Bodi inakaribisha maombi ya kazi ya Udereva kwa mkataba katika ofisi za Bodi zilizoko Dar es Salaam, Dodoma and Mbeya

Sifa Za Mwombaji

Mwombaji anatakiwa kuwa na cheti cha kuhitimu kidato cha nne(Certifcate of Secondary Education), Cheti cha mafunzo ya awali ya udereva kutoka chuo kinachotambulika na VETA, leseni ya udereva daraja “C” na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua miaka mitatu bila kusababisha ajali.

Pia muombaji anatakiwa kuwa na cheti cha majaribio ya ufundi wa magari, daraja la pili, kutoka VETA pamoja na cheti cha udereva mahiri daraja la pili kutoka chuo cha Taifa cha Usafirishaji(NIT)

Majukumu ya kazi

·         Kuendesha gari la Taasisi

·         Kutunza na kuandika daftari la safari(log-book) kwa safari zote

·         Kufanya uchunguzi wa gari kabla ya safari ili kugundua ubovu unaohitaji matengenezo

·         Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari

·         Kuhakikisha gari na vyombo vyake vipo katika hali nzuri wakati wote

·         Kutekeleza kazi nyingine yoyote atakayopangiwa na mkuu wake wa kazi

Mshahara

Kwa kuzingatia viwango vya mishahara ya bodi

Masharti kwa Muombaji

·         Muombaji awe raia wa Tanzania

·         Muombaji awe na umri usiozidi miaka 35

·         Barua ziambatanishwe na vyeti husika ambavyo vimethibitishwa na mwanasheria na maelezo binafsi ya muombaji(CV), yaliyosainiwa

·         Barua ziwe na anwani na namba za simu za kuaminika

·         Majina, anwani na simu za wadhamini wawili wanaomtambua muombaji

Maombi yatumwe kwa anwani ifuatayo

Kaimu Msajili

Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi

S.L.P 72673, Simu 2110292, Jengo la Tetex, Ghorofa ya Pili, Dar es Salaam

 

Barua Pepe: info@aqrb.go.tz

More Jobs From This Company

Overview

  • Location: Dar es Salaam, Dodoma, Mbeya
  • Job Title: Dereva
  • Application Deadline: 2018-01-05
Login to Quick Apply

Apply For This Job

Upload your CV (optional) Max. file size: 5MB
No file selected


Sharing is caring

×

Login

×

Apply Now

Please choose how you are going to apply for this post


×

Apply Now