Msimamizi wa Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Taasisi
THE NATIONAL SPIRITUAL ASSEMBLY OF THE BAHA'IS OF TANZANIA
Kiziba Village, Kigoma Rural District, Kigoma Region, Tanzania
Contractual
9th January 2026
TANGAZO LA NAFASI YA KAZI
NAFASI - 1: Msimamizi wa Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Taasisi.
1. Utangulizi
Baraza la Kiroho la Kitaifa la Wabaha’i wa Tanzania ni taasisi ya dini iliyo na usajili rasmi wa kutekeleza shughuli zake za kidini hapa Tanzania. Baraza linatangaza nafasi moja ya kazi ya Msimamizi wa Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Taasisi. Lengo la nafasi hii ni kuhakikisha kuwa utekelezaji wa mradi wa ujenzi unafanyika kwa ubora unaotakiwa, kwa wakati, na kwa kuzingatia bajeti, sheria, pamoja na taratibu zote husika za ujenzi. Mradi huu unatekelezwa katika Kijiji cha Kiziba, Wilaya ya Kigoma Vijijini, Mkoa wa Kigoma.
2. Majukumu Makuu
Msimamizi wa Mradi atakuwa na wajibu wa:
- Kusimamia utekelezaji wa mradi wa ujenzi kwa kuzingatia michoro, makubaliano ya mkataba, na ratiba ya kazi.
- Kusimamia na kuratibu kazi za wakandarasi, mafundi, na washauri wa mradi.
- Kufuatilia maendeleo ya mradi na kuhakikisha ubora wa kazi unazingatia viwango vilivyokubalika na sheria za nchi za ujenzi na mahitaji ya taasisi.
- Kuhakikisha viwango vya usalama na afya kazini vinafuatwa katika eneo la mradi.
- Kuandaa na kuwasilisha taarifa za maendeleo ya mradi (kiufundi na kiutendaji) kwa uongozi wa taasisi kwa wakati.
- Kuripoti changamoto zinazojitokeza na kupendekeza njia za kuzitatua kabla changamoto hizo hazijaleta madhara kwenye mradi.
3. Sifa za Mwombaji
- Elimu ya Astashahada au Stashahada katika Uhandisi wa Ujenzi wa majengo, Usanifu Majengo (Architecture), Usimamizi wa Miradi ya ujenzi wa majengo, au fani inayohusiana.
- Uzoefu usiopungua miaka mitatu (3) katika kusimamia miradi ya ujenzi wa majengo ya taasisi.
- Uzoefu wa awali katika miradi ya ujenzi wa majengo ya makazi au ya taasisi utazingatiwa zaidi.
- Uelewa wa sheria za ujenzi, kanuni za mipango miji, na viwango vya kitaifa vya ujenzi.
- Ujuzi wa usimamizi wa mikataba, ratiba za kazi za ujenzi.
4. Ujuzi na Uwezo Binafsi
- Uwezo mzuri wa uongozi, usimamizi wa watu, na kufanya kazi na timu.
- Uwezo mzuri wa mawasiliano ya maandishi na ya mdomo.
- Uadilifu, uwajibikaji, na maadili mema ya kazi.
- Uwezo wa kufanya kazi bila shinikizo na kutatua changamoto kwa ufanisi.
5. Masharti ya Ajira
- Nafasi hii ni ya mkataba kwa kipindi kitakachobainishwa na taasisi.
- Mshahara na stahiki nyingine zitalipwa kulingana na taratibu za taasisi.
- Mkazi wa Mkoa wa Kigoma au maeneo ya karibu atapewa kipaumbele.
- Awe tayari kuishi vijijini (sehemu ulipo ujenzi)
- Awe na afya njema na awe tayari kuwepo eneo la mradi muda wote.
6. Jinsi ya Kutuma Maombi
Waombaji wenye sifa wanatakiwa kuwasilisha:
- Barua ya maombi.
- Wasifu binafsi (CV) unaoonyesha elimu, uzoefu wa kazi, na maelezo ya wadhamini (referees). (Nakala zote ziwe katika pdf file moja).
- Maombi yawasilishwe kwa maandishi kupitia barua pepe (secretariat@bahai.or.tz) kabla ya tarehe 09/01/2026
7. Maelezo ya Ziada
Ni waombaji waliokidhi vigezo watakaowasiliana kwa hatua zinazofuata za usaili.