Mwendesha Wa Mashine (Machine Operators) Western Hauliers Dar es Salaam, Tanzania
Full-Time
30th September 2025

Mwendesha Wa Mashine

Maelezo ya Kazi

Kampuni: Western Hauliers Ltd.

Eneo: Dar es Salaam, Tanzania (pamoja na safari za mikoani)

Anaripoti kwa: Meneja wa Uendeshaji / Msimamizi wa Mashine/ Magari

Muhtasari wa Nafasi

Oparesheni wa Mashine anawajibika kuendesha mashine za kampuni kwa usalama, ufanisi na weledi. Hii inahusisha malori, kreni, forklift, box loaders na manlift. Nafasi hii inalenga kuhakikisha utekelezaji wa huduma za kunyanyua, kurig, kusafirisha na shughuli nyingine za usafirishaji kwa kufuata taratibu za Western Hauliers, mahitaji ya wateja na kanuni za usalama.

Majukumu Makuu

  • Kuendesha mashine/kifaa kilichopangiwa kwa usalama na ufanisi kwa kufuata taratibu za kampuni.
  • Kufanya ukaguzi wa kila siku kabla na baada ya kuendesha mashine na kuhakikisha taarifa zinaandikwa.
  • Kuripoti mara moja hitilafu, uharibifu au mahitaji ya matengenezo.
  • Kufuata viwango vya usalama ikiwemo kutumia PPE na kufuata kanuni za maeneo ya wateja.
  • Kutekeleza majukumu ya kunyanyua, kurig, kupakia, kusafirisha au kupakua kulingana na maagizo ya kazi.
  • Kushirikiana na marigga, wasimamizi na wateja ili kuhakikisha nafasi sahihi na usalama wa mizigo.
  • Kuhifadhi kumbukumbu sahihi za safari, matumizi ya mafuta na ukamilishaji wa kazi.
  • Kuhakikisha mizigo imefungwa vizuri na kufuata kanuni za barabarani/usafirishaji.
  • Kudumisha weledi, muda sahihi na uaminifu katika kushughulika na wateja.

Sifa na Ujuzi

  • Leseni halali ya kuendesha mashine husika.
  • Uzoefu wa angalau mwaka 1 wa kuendesha mashine nzito.
  • Uelewa mzuri wa matengenezo ya mashine, ukaguzi na taratibu za usalama.
  • Uwezo mzuri wa mawasiliano (Kiswahili na Kiingereza vinapendelewa).
  • Uwezo wa kufuata maagizo, kufanya kazi chini ya shinikizo na kukamilisha kazi kwa wakati.
  • Awe na afya njema na kuzingatia usalama.

Viashiria Vikuu vya Utendaji (KPIs)

  • Hakuna ajali au uvunjaji wa kanuni za usalama.
  • Kufuata muda na ratiba.
  • Kukamilisha kwa usahihi fomu za ukaguzi wa mashine na kumbukumbu za kazi.
  • Kufuata sera za kampuni (matumizi ya PPE, kuripoti, mawasiliano).
  • Kuridhika kwa mteja na utoaji wa huduma.

Masharti ya Kazi

Kituo cha kazi kitakuwa Dar es Salaam, pamoja na safari za mikoani na kuvuka mipaka (Zambia, DRC, n.k.). Kazi inaweza kuhusisha masaa marefu, wikiendi na sikukuu kulingana na mahitaji ya uendeshaji.

Malipo na Manufaa

Mfanyakazi atakayechaguliwa atanufaika na mshahara mzuri, malipo ya posho ya kutosha, bima ya afya, na mazingira rafiki ya kazi.

CV na vyeti vitumwe kupitia;-

WhatsApp kupita namba 0677 151 000

Au barua pepe admin@westernhauliers.co.tz

NB: Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 30.09.2025

Application
Login to Quickly Apply