FURSA YA KAZI
WAKALA WA USAJILI HUDUMA YA FAIBA
TTCL Corporation
Shirika la Mawasiliano Tanzania - TTCL Corporation linakaribisha vijana wenye uwezo kwa ajili ya kazi ya Uwakala wa usajili wa wateja wa Faiba katika jiji la Dar es salaam.
1. SIFA ZA WAOMBAJI
Umri usiopungua miaka 18.
Awe raia wa Tanzania mwenye kitambulisho halali kimoja au zaidi kati ya vifuatavyo; Kitambulisho cha Taifa (NIDA), Kitambulisho cha Mpiga Kura,leseni ya Udereva, au kitambulisho kingine kinachotambulika kisheria.
Awe na cheti cha kuhitimu Kidato cha Nne.
Awe anaishi Dar es salaam.
Awe na uwezo wa kusoma na kuandika Kiswahil na /au Kiingereza.
Awe na nidhamu, uadilifu, na asiwe na rekodi ya makosa yoyote ya jinai au mashtaka yanayohusiana na uaminifu.
Awe na uwezo wa kutumia simu janja (smartphone) kwa shughuli za kijidigitali.
Awe tayari kupokea mafunzo na kufuata taratibu za Shirika.
Awe na uwezo wa kujieleza na kuwasiliana na wateja.
2. TARATIBU ZA MAOMBI
Waombaji wote wafike TTCL Kijitonyama, wilaya ya Kinondoni, Dar es salaam tarehe 16/12/2025 kuanzia saa 03:00 asubuhi kwa ajili ya usahili wakiwa na viambatanishi elekezi.
Kwa taarifa zaidi tafadhali wasiliana nasi kupitia 0222 100 100 au barua pepe: dg@ttcl.co.tz